Riyadh. Rais wa Palesina afanya mazungumzo na Mfalme Abdullah.
29 Julai 2006Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amewasili nchini Saudi Arabia leo kwa mazungumzo na mfalme Abdullah kuhusiana na mzozo wa sasa wa mashariki ya kati.
Abbas ambaye yumo katika ziara ya mataifa ya Kiarabu kutafuta kuungwa mkono wakati Israel inaendelea na mashambulizi yake makubwa dhidi ya ukanda wa Gaza , atabadilishana mawazo na mfalme Abdullah juu ya hali ya hatari iliyoko katika eneo hilo na kumfahamisha kiongozi huyo wa Saudia kuhusu hali ya mambo katika maeneo ya Palestina.
Abbas amewasili akitokea nchini Misr , na pia anatarajiwa kufanya ziara nchini Kuwait kesho Jumapili na Qatar siku ya Jumatatu.
Israel imekuwa ikifanya mashambulizi makubwa ya uharibifu dhidi ya Gaza na Lebanon kufuatia kukamatwa kwa wanajeshi wake na wapiganaji wa Hizbollah na Wapalestina.