RIYADH : Polisi apigwa risasi na kuuwawa Mecca
30 Oktoba 2005Matangazo
Watu wawili wenye silaha wamempiga risasi na kumuwa polisi mmoja katika mji mtakatifu wa Mecca jana usiku.
Tukio hilo limetokea katika eneo moja la mji huo magharibi ya Saudi Arabia ambapo zaidi ya waumini milioni moja na nusu wa Kiislam wamekusanyika kuadhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhani.Washambuliaji hao wawili walifyetulia risasi doria ya polisi ambayo ilikuwa imewaashiria wasimamishe gari lao kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida.
Mmojawapo wa polisi hao wawili alikuwa amepigwa risasi kichwani.