RIYADH: Mfalme Fahd wa Saudi Arabia atibiwa hospitali
28 Mei 2005Matangazo
Hali ya siha ya Mfalme Fahd wa Saudi Arabia,sasa imedhibitiwa.Kwa mujibu wa maafisa nchini Saudi Arabia,Mfalme Fahd alitolewa maji kwenye mapafu,baada ya kupelekwa hospitali akiwa na nimonia.Mfalme Fahd mwenye umri wa miaka 82,ni mfalme wa Saudi Arabia tangu mwaka 1982 lakini amekuwa akiumwa kwa miaka mingi.Mnamo mwaka 1995 aliuugua kiharusi na tangu wakati huo ni Mwana Mfalme Abdullah anaetekeleza shughuli za kifalme.