RIYADH: Mfalme Fahd wa Saudi Arabia apelekwa hospitali
28 Mei 2005Matangazo
Hali ya wasi wasi imezuka nchini Saudi Arabia baada ya Mfalme Fahd kupelekwa hospitali kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.Ripoti zisizo rasmi zimesema hali ya tahadhari imetangazwa,lakini baadae serikali ilikanusha ripoti hiyo.Shirika rasmi la habari SPA limesema hali ya Mfalme Fahd ni nzuri na uchunguzi wa siha yake ulikamilishwa kama kawaida.Mfalme Fahd mwenye umri wa miaka 82,ni mfalme wa Saudi Arabia tangu mwaka 1982 lakini amekuwa akiumwa kwa miaka mingi.Mnamo mwaka 1995 aliuugua kiharusi na tangu wakati huo ni Mwana Mfalme Abdullah anaetekeleza shughuli za kifalme.