RIYADH: Hatari mapigano kuenea Mashariki ya Kati
25 Julai 2006Matangazo
Mfalme Abdallah wa Saudi Arabia ameonya kuwa vita vitasambaa kote Mashariki ya Kati,ikiwa Israel itaendelea kuishambulia Lebanon na Wapalestina. Vile vile ametoa mwito wa kusitisha mapigano.Si kawaida kwa matamshi kama hayo kutoka Saudia Arabia.Wakati huo huo kundi la wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon limelaumiwa kuanzisha mapambano.Taarifa hiyo,inatazamwa kama ni mwito kwa Marekani.Serikali ya Riyadh inaamini kuwa Marekani ni nchi pekee yenye uwezo wa kuishawishi Israel isitishe mashambulio yake.Ripoti zasema kuwa Saudi Arabia imeahidi kutoa msaada wa Dola milioni 500 kuijenga upya Lebanon na Dola milioni 250 kwa ajili ya Wapalestina.