Marekani: Ujerumani ilikiuka haki za binaadamu, 2024
13 Agosti 2025Matangazo
Muhtasari wa ripoti hiyo umeonyesha kuwa Hali ya haki za binadamu nchini Ujerumani ilidorora sana mwaka 2024, na hasa kwenye masuala muhimu ya haki za binadamu yaliyojumuisha vikwazo vya uhuru wa kujieleza na ripoti za kuaminika za uhalifu, vurugu au vitisho vya vurugu vinavyochochewa na chuki.
Ripoti hiyo lakini imesema, serikali ya Ujerumani "ilichukua hatua za kuaminika kuchunguza, kuwashtaki na kuwaadhibu maafisa waliofanya matukio hayo.
Hata hivyo, wataalamu wa haki za binaadamu wanaikosoa ripoti hiyo ambayo huko nyuma ilichukuliwa kama rejea ya kutegemewa katika utetezi wa haki za binadamu duniani, wakisema imepotoshwa na kuacha mambo mengi ili kuendana na malengo ya kisiasa ya utawala wa sasa.