Ripoti ya awali kuhusu ajali ya ndege ya Air India yatolewa
12 Julai 2025Ripoti hiyo, iliyotolewa leo na Ofisi ya Uchunguzi wa Ajali za Ndege ya India, pia imeeleza kuwa rubani mmoja alisikika kupitia kinasa sauti cha chumba cha marubani akimuuliza mwenzake kwanini alikatiza mafuta kwenye ndege katika dakika za mwisho mwisho kabla ya ndege kuanguka, lakini akajibu kuwa hakufanya hivyo.
Kisanduku cha mawasiliano ya ndege ya Air India chapatikana
Ripoti hiyo ilizingatia matokeo yake kwenye data iliyopatikana kutoka kwa visanduku vyeusi vya ndege hiyo ambavyo hunasa sauti za marubani na kurekodi data za safari ya ndege.
Ndege hiyo yaAir India aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, ilianguka mnamo Juni 12 na kuwauwa takriban watu 260 ikiwa ni pamoja na wengine 19 waliokuwa katika eneo ilikoanguka kwenye mji wa Ahmedabad kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Ni mtu mmoja tu aliyenusurika ajali hiyo ambayo ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea katika sekta ya safari za angani nchini India.