Migogoro
Ripoti: Vita vitapoteza makaazi ya watu milioni 6.7
14 Machi 2025Matangazo
Haya yamesemwa leo na shirika la misaada ya Kibinadamu la Baraza la Wakimbizi la Denmark, DRC.
DRC, imesema kukatizwa kwa misaada ya kimataifa na Marekani, Uingereza na Ujerumani kumewaacha mamilioni ya watu wenye uhitaji bila msaada muhimu.
Katika taarifa, Katibu Mkuu wa DRC Charlotte Slente, amesema dunia inaishi katika nyakati za vita na hali ya kutojali sheria, huku raia wakiathirika zaidi.
DRC imesema idadi ya watu waliopoteza makazi yao duniani kote kwa sasa ni milioni 122.6.
Shirika hilo linakadiria kuwa watu milioni 4.2 wanatarajiwa kupoteza makaazi yao ulimwenguni kote kwa mwaka huu wa 2025, haya yakiwa makadirio ya juu zaidi ya DRC tangu 2021.
Watu wengine milioni 2.5 wanatarajiwa kuyapoteza makazi yao kwa lazima ifikapo mwaka 2026.