MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
M23 na jeshi la Kongo wahusishwa na ukiukaji wa haki DRC
5 Septemba 2025Matangazo
Kwa mujibu wa ripoti ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, kuna uwezekano kulifanyika uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya mambo katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, imebaini kuwa pande zote katika mzozo huo zimehusika pakubwa katika ukiukaji wa haki za binadamu tangu mwishoni mwa mwaka 2024, yakiwemo mauaji ya kiholela, kutoweka kwa raia na ukatili wa kingono.
Eneo la Mashariki mwa Kongo, linalopakana na Rwanda na lenye raslimali nyingi za asili na utajiri wa madini, limekumbwa na machafuko kwa zaidi ya miongo mitatu.