Ripoti: Israel kuruhusu mashirika kusambaza misaada Gaza
6 Julai 2025Matangazo
Taarifa hizo ni kwa mujibu wa gazeti la Times of Israel la leo. Msemaji wa serikali alikataa kutoa maoni kuhusu taarifa hiyo, lakini Waziri wa Fedha kutoka mrengo wa kulia, Bezalel Smotrich, alichapisha kwenye ukurasa wake wa X (zamani Twitter) akisema kuwa Baraza la Mawaziri limefanya "uamuzi mbaya". Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, Israel iliunga mkono hatua ya Shirika lenye utata la Gaza Humanitarian Foundation (GHF) kusambaza misaada, kwa madai kuwa kundi la Hamas limekuwa likitumia misaada hiyo kwa maslahi yake ya kijeshi. Marekani pia imeunga mkono mfumo huo mpya, lakini Umoja wa Mataifa umeukosoa vikali.