Ripoti: Idadi kubwa ya watu duniani wanavuta hewa chafu
11 Machi 2025Haya ni kulingana na ripoti iliyochapishwa jana na kampuni ya ufuatiliaji ubora wa hewa, IQAir, yenye makao yake nchini Uswisi.
IQAir ilichambuwa data kutoka vituo 40,000 vya ufuatiliaji ubora wa hewa katika nchi 138 na kugundua kuwa Chad, Kongo, Bangladesh, Pakistan na India zilikuwa na viwango vya juu zaidi vya hewa chafu.
India ilikuwa na miji sita kati ya tisa iliyo na hewa chafu zaidi huku mji wa viwanda wa Byrnihat ukiathirika zaidi.
Wataalamu wanasema kiwango halisi cha uchafuzi wa hewa kinaweza kuwa kikubwa zaidi kwa sababu sehemu nyingi za dunia hazina ufuatiliaji unaohitajika kwa usahihi zaidi wa data.
Barani Afrika kwa mfano, kuna kituo kimoja tu cha ufuatiliaji kwa kila watu milioni 3.7
Shirika la Afya Duniani, WHO, linakadiria kuwa uchafuzi wa hewa husababisha vifo vya takribani watu milioni 7 kila mwaka.