Riadh: Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Saud Arabia polisi...
26 Novemba 2003Matangazo
imefanikiwa kuepusha balaa la ashambulio la mabomu yaliyofichwa ndani ya gari nchini humo.Televisheni ya Suudia imesema magaidi wawili wameuwawa katika mapambano pamoja na polisi.Gari yao imegunduliwa na shehena kubwa ya baruti.Watu wasiopungua 18 waliuliwa mapema mwezi huu katika shambulio moja dhidi ya makaazi ya wageni katika mtaa moja wa mjini Ryadh.Na nchini Yemen duru rasmi zinasema dhamana mmojawapo wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaida nchini humo,Mohammed Hamdi el Ahdal ametiwa mbaroni.