RATIBA YA SERIKALI YA MPITO IRAQ
25 Novemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Baraza Tawala la Wairaqi lililochaguliwa na Marekani,limepeleka Umoja wa Mataifa ratiba inayoeleza hatua za kuundwa serikali ya mpito nchini Iraq.Baraza hilo limearifu kuwa hadi 31 Mei mwaka ujao,litawachagua wajumbe wa muda.Wajumbe hao mwishoni mwa mwezi Juniwataiteua serikali ya mpito.Na uchaguzi mkuu wa kuichagua serikali mpya ya Iraq utafanywa mwishoni mwa mwaka 2005.