BiasharaAfrika Kusini
Ramaphosa: Tunatafuta masoko mapya Afrika na Asia
4 Agosti 2025Matangazo
Ramaphosa, amesema kuwa ukweli ni kwamba, Afrika Kusini sio taifa pekee linalopambana na mgogoro huu bali mataifa mengine mengi yamo kwenye hali mbaya hata kuliko Afrika Kusini na kwamba nchi zote ziko kwenye mchakato wa mazungumzo ya kufikia makubaliano na Marekani.
Rais huyo wa Afrika Kusini amesema kwa sasa kipaumbele cha nchi yake ni kuilinda sekta ya mauzo ya nje na kuendelea kuyafikia masoko ya bidhaa zake.
Ushuru wa Marekani unaziweka hatarini karibu ajira 30,000 mamlaka za Afrika Kusini zimesema Jumatatu, siku nne kabla ya suhuru wa asilimia 30 iliowekewa na Marekani kuanza kutekelezwa.