Ramaphosa azungumza na Kagame kuhusu vita vya Goma
28 Januari 2025Matangazo
Ramaphosa na Kagame wamekubaliana juu ya hitaji la dharura la kusitishwa kwa mapigano na kuanzishwa tena kwa mchakato wa mazungumzo ya amani kwa kuzijumuisha pande zote zinazohusika.
Haya yanajiri wakati Rais wa Kenya William Ruto akitangaza kuwa Kagame na Rais wa Kongo Felix Tshisekedi watahudhuria hapo kesho mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huku Umoja wa Afrika ukikutana pia hivi leo ili kuujadili mzozo huo.
Soma pia:Waasi wa M23 waingia Goma
Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa waasi wa M23 wamechukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa Goma.