Ramaphosa aonya kuhusu kitisho cha amani duniani
26 Februari 2025Matangazo
Ramaphosa ametoa tahadhari hiyo kwenye ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa mataifa tajiri na yanayoinukia kiuchumi la G20 nchini Afrika Kusini, unaoendelea bila ya Waziri wa Fedha wa Marekani.
Pamoja na onyo hilo, amesema kuna umuhimu mkubwa wa kufuata taratibu zinazozingatia sheria kama njia ya kudhibiti na kutatua migogoro wakati huu wa ushindani wa siasa za kimaeneo.
Mkutano huu unafunguliwa wiki moja baada ya ule wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa G20, ambapo pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio hakuhudhuria, akilalamikia ajenda za nchi hiyo zinazoipinga Marekani.