Ramaphosa akosoa ziara ya AfriForum nchini Marekani
28 Februari 2025Ziara hiyo imefanyika katika wakati ambapo mivutano imeongezeka kati ya Afrika Kusini na utawala wa Rais Donald Trump. Jana Rais Ramaphosa, akizungumza na vyombo vya habari, alisema Afrika Kusini inajaribu kutafuta makubaliano na Trump kumaliza mkwamo unaoendelea na serikali yake, lakini pia akasema kitendo kilichofanywa na viongozi wa kundi la washawishi wa jamii ya Afrikaner la AfriForum kinakwenda kinyume na ari ya ujenzi wa taifa.
Ramaphosa amesema ziara ya viongozi hao wa jamii ya wazungu walio wachache nchini Afrika Kusini katika ikulu ya White House, inatengeneza zaidi migawanyiko kuliko kuijenga Afrika Kusini.
Trump amedai kwamba serikali ya Afrika Kusini inawapokonya Waafrika Kusini Wazungu ardhi yao kupitia sheria yake mpya ya kusimamia umiliki wa ardhi.