Ramallah:Israel yawauwa wapalestina katika msako wa nyumba hadi nyumba.
22 Agosti 2006Matangazo
Vikosi vya kijeshi vya Isreal wakisaidiwa na helikopta za kijeshi, vifaru na magari yenye silaha wameelekea maeneo yanayomilikiwa na wa-Palestina na kufanya msako wa nyumba kwa nyumba na kuwakamata kadhaa.
Jeshi limesema wanajeshi wameizunguuka nyumba na wakawa wanarushiana risasi na wanamgambo wa kipalestina wakiwemo wanachama wawili wa chama cha Hamas ambao walikuwemo ndani ya nyumba hiyo.
Mmoja kati ya wanamgambo hao amejeruhiwa na watano waliobakia wamekamatwa.
Huko kusini mwa Gaza wanamgambo watatu wa kipalestina wameripotiwa kuuwawa katika mapigano na wanajeshi wa Israel.