Raiya wawili wa Kiingereza wauawa Iraq:
28 Machi 2004Matangazo
BAGHDAD:
Nchini Iraq wameuawa raiya wawili wa Kiingereza katika shambulio lililofanywa Kaskazini ya nchi. Watu waliovalia vinyago waliwapiga risasi wanaume hao wawili waliokuwa njiani katika gari yao mjini Mossui. Waingereza hao walikuwa wakiushughulikia mfumo wa kukarabati usambazaji wa umeme kwa niaba ya kampuni ya Kiingereza. Mjini Bakuba walijeruhiwa raiya watano wa Kiiraq, wakiwemo watoto wawili. Shambulio hilo walikusudiwa wanachama wa Kikosi cha Hifadhi ya Raiya. Tangu Ijumaa wamekwisha uawa watu 21 nchini Iraq, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.