MigogoroUkraine
Rais Zelensky asema amekuwa na mazungumzo mazuri na Trump
26 Aprili 2025Matangazo
"Kwa kweli tumekuwa na mkutano wenye tija sana. Bila shaka, ni kuhusu jinsi ya kuleta amani na tunataka kuendelea na mikutano kama hiyo ili kuleta amani nchini Ukraine," alisema Zelenskyy
Taarifa nyingine kutoka mjini Moscow zimesema Rais Vladimir Putin wa Urusi ameelezea kwa mara nyingine utayari wa mazungumzo na Ukraine bila ya masharti yoyote ya awali, wakati wa mkutano na mjumbe maalumu wa Trump, Steve Witkoff jana Ijumaa.
Shirika la habari la Urusi la Interfax limearifu hii leo likimnukuu msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov.