Rais Zelensky amuomba Trump aitembelee Ukraine
14 Aprili 2025Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amemtolea mwito Rais Donald Trump wa Marekani kuitembelea nchi yake ili kujionea mwenyewe janga lililosababishwa na vita vinavyoendelea, vilivyoanzishwa na Urusi, kabla ya kukubaliana na suluhu yoyote ya amani iliyopendekezwa na Urusi.Soma pia: Viongozi wa dunia walaani shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine
Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo kimoja cha utangazaji nchini Marekani cha CBS, Zelensky amemuomba Trump kwenda kuwatazama raia wa Ukraine, hospitali, makanisa yaliyoharibiwa, watoto waliopata madhara au waliokufa kutokana na vita hivyo.
Mahojiano hayo ya Zelensky yalichapishwa jana Jumapili chini ya kiwingu cha shambulio kubwa la roketi lililofanywa na Urusi dhidi ya mji wa Sumy ambako kiasi watu 34 waliuwawa.