SiasaUkraine
"Ulaya,Marekani zihusishwe kwenye mchakato wa amani Ukraine"
25 Januari 2025Matangazo
Zelenskiy ameyasema hayo siku ya Jumamosi katika mkutano wa pamoja na Rais wa Moldova Maia Sandu ambaye yuko ziarani mjini Kyiv, na kuongeza kuwa ili mazungumzo hayo yawe na ufanisi, Ukraine inahitaji pia kushirikishwa.
Rais Sandu amesema Moscow inalenga kuchochea mzozo wa kijamii na kiuchumi huko Moldova katika dhamira ya kuwaweka vibaraka wao madarakani. Rais Zelenskiy na mwenzake wa Moldova wamejadiliana pia kuhusu mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushirikiano katika sekta ya nishati kwa lengo la kupunguza bei ya umeme kwa asilimia 30 huko Moldova.