SiasaKorea Kusini
Rais Yoon wa Korea Kusini aliyekuwa kizuizini ameachiliwa
8 Machi 2025Matangazo
Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap limeripoti leo kuwa rais wa Korea Kusini aliyeko kizuizini Yoon Suk Yeol ameachiliwa hii leo baada ya waendesha mashtaka nchini humo kuamua kutokata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kumuondoa kizuizini.
Hapo jana mahakama ya Korea Kusini iliamuru kuachiliwa kwa Rais Yoon Suk Yeol hatua iliyochukuliwa kwamba inaweza kumruhusu Yoon kujibu mashtaka yake ya uasi bila kuwa kizuizini.
Soma zaidi. Mahakama ya Seoul yaamuru rais Yoon kuachiwa huru
Yoon alikamatwa na kufunguliwa mashtaka Januari 3 juu ya sheria yake ya kuweka nchi chini ya sheria ya kijeshi ya Desemba 3 na ambayo iliingiza nchi hiyo katika machafuko ya kisiasa.