Rais Xi Jinping wa China yuko ziarani Cambodia
17 Aprili 2025Xi anabeba ujumbe wa ushirikiano wa karibu na kulinda maslahi ya pamoja katika ziara hiyo.
Katika makala aliyoandika na kuchapichwa kwenye vyombo vya habari vya Cambodia kabla ya kuwasili kwake, Xi ameirai nchi hiyo kushirikiana na China kupambana dhidi ya "mfumo unaotegemea nguvu za taifa moja duniani, siasa za mabavu na mivutano isiyo na tija."
Amesema nchi hizo mbili ni lazima zikatae sera za kufunga milango na badala yake zipigie debe kuendeleza ushirikiano katika ngazi ya kimataifa.
Cambodia iliyo msafirishaji mkubwa wa nguo kwenda Marekani, iliwekewa ushuru wa asilimia 49 na utawala wa Donald Trump ambao umeshitishwa kwa muda hadi mwezi Julai. Viongozi wa nchi hiyo wanatumai ziara ya Xi itasaidia kupatikana msaada zaidi wa kifedha ikiwemo miundombinu.