SiasaUrusi
Rais Xi wa China afanya mazungumzo na Rais wa Putin
8 Agosti 2025Matangazo
Shirika la habari la China, CCTV, limeripoti kwamba Xi alizungumza na Putin kwa njia ya simu hii leo, kufuatia ombi la Putin, aliyemuarifu kuhusu "hali ya mawasiliano ya hivi karibuni" kati ya Marekani na Urusi, pamoja na hali ya Ukraine.
Idara ya Kiingereza ya shirika la habari la China, Xinhua, ilimnukuu Xi akimweleza Putin kuhusu kuridhishwa na hatua ya kuimarisha uhusiano na namna wanavyohamasiha suluhu la kisiasa kwenye mgogoro wa Ukraine.
Putin na Rais Donald Trump wa Marekani wanatarajiwa kufanya mazungumzo wiki ijayo ya kujaribu kuvimaliza vita nchini Ukraine.