Sheria na HakiUlaya
Rais wa zamani Ufilipino Duterte ashikiliwa na ICC
13 Machi 2025Matangazo
Mahakama hiyo inatarajiwa katika kipindi cha siku kadhaa zijazo kuanza vikao vya awali vya kesi hiyo,vya kuthibitisha uwepo mahakamani wa mtuhumiwa, kutaja mashataka pamoja na kutangaza tarehe ya kuanza kusikiliza kesi,na kutathmini ikiwa waendesha mashataka wana ushahidi wa kutosha wa kumfungulia kesi kamili.
Soma pia:Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte akamatwa kwa warranti wa ICC
Jana mahakama hiyo ilimpokea rais huyo wa zamani wa Ufilipino aliyekamatwa kufuatia warranti wa mahakama hiyo,inayomtuhumu kwa uhalifu wa ubinadamu,kutokana na kampeini aliyoianzisha akiwa madarakani ya kukabiliana na biashara ya madawa ya kulevya, iliyosababisha maelfu kuuliwa nchini Ufilipino.