SiasaAsia
Rais wa zamani wa Ufilipino kupelekwa ICC
11 Machi 2025Matangazo
Amesema atasafirishwa kwa ndege itakayoondoka leo jioni kufuatia kukamatwa kwake leo asubuhi kwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Katika taarifa, Sara amesema hatua iliyochukuliwa dhidi ya baba yake sio ya haki na ameitaja kuwa dhuluma na mateso.
Sara ameongeza kuwa baba yake ameshindwa kudai haki yake mbele ya mamlaka za mahakama nchini humo.
Mapema, Duterte alikuwa amesema kuwa anapaswa kufunguliwa mashtaka katika mahakama za Ufilipino na sio ile ya ICC.
Waranti wa ICC ulioonekana na shirika la habari la Reuters, unamshtumu Duterte kwa mauaji ya takribani watu 43 kati ya mwaka 2011-2019 kama sehemu ya vita vyake dhidi ya dawa za kulevya.