Rais wa zamani wa Ufilipino akamatwa chini ya waranti wa ICC
11 Machi 2025Kukamatwa kwake ni kutokana na waranti ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC, kuhusiana na kesi ya uhalifu dhidi ya ubinadamu iliyowasilishwa dhidi yake. Haya ni kwa mujibu wa serikali ya nchi hiyo.
Katika taarifa, ofisi ya Rais Ferdinand Marcos imesema kuwa Duterte alikamatwa baada ya kuwasili kutoka Hong Kong na kuwekwa kizuizini kwa amri ya ICC ambayo imekuwa ikichunguza mauaji ya watu wengi yaliyotokea chini ya msako mkali dhidi ya dawa za kulevya.
Mmoja wa wakili wa Duterte Silvestre Bello III amesema "Ninahisi kwamba amenyimwa haki zake za kisheria, hasa kama rais wa zamani. Hata kama utapuuza hilo...kwa mtu yeyote, Mfilipino, una haki ya kupata haki zote za kikatiba kama ilivyowekwa katika katiba yetu."
Kukamatwa kwa Duterte kumezishangaza familia za waathiriwa wa msako huo wa kikatili ambazo zimeelezea kushukuru kwamba hatimaye haki imetendeka.