JangaNigeria
Rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari azikwa
16 Julai 2025Matangazo
Maelfu ya Wanigeria walikusanyika kwa ibada ya mazishi kwenye mji huo kabla ya mwili wa Buhari kuzikwa kwenye makaburi ya familia.
Rais wa sasa wa Nigeria Bola Tinubu, Umaro Sissoco Embaló wa Guinea Bissau, na Waziri Mkuu wa Niger, Ali Lamine Zeine ni miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu na watu mashuhuri walioshiriki mazishi hayo.
Buhari aliyekuwa na umri wa miaka 82, aliaga dunia siku ya Jumapili mjini London wakati akipatiwa matibabu ya maradhi ambayo hayajawekwa wazi.