SiasaKorea Kusini
Rais wa zamani wa Korea Kusini akaidi kuhojiwa
1 Agosti 2025Matangazo
Mwendesha mashtaka Oh Jeong-hee amesema rais Suk Yeol alilala kwenye chumba chake cha gereza akiwa amevalia nguo yake ya ndani pekee na hivyo maafisa wakashindwa kumhoji.
Waendesha mashitaka walimweleza rais Yoon kwamba katika jaribio linalofuata la kumhoji, watalazimika kutumia nguvu ikiwa itahitajika.
Rais huyo alieondolewa alikamatwa baada ya kujaribu kutangaza sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3, hatua iliyoitumbukiza nchi hiyo katika machafuko ya kisiasa, na sasa anakabiliwa na mlolongo wa mashtaka, ikiwa ni pamoja na uasi, kuvuruga uchaguzi, lakini mara kadhaa amekuwa akikaidi kuhojiwa na mahakama.