Rais wa zamani wa Iran Rafsaanjani anapanga kutetea upya wadhifa huo
11 Mei 2005Matangazo
Rais wa zamani wa Iran Ali Akbar Hashemi Rafsanjani ameamua kutetea kwa mara nyengine tena wadhifa huo wa juu kabisa nchini mwake.Mwanasiasa huyo mwenye umri wa amiaka 70 ametangaza rasmi azma hiyo.Anapewa nafasi nzuri ya kushika nafasi inayoachwa na rais mpenda mageuzi Mohammed Khatami.Baada ya awamu mbili madarakani rais Mohammed Khatami haruhusiwi kutetea tena wadhifa huo.Watetezi wa kiti cha urais wameanza kujiandikisha tangu jana.Zoezi hilo litaendelea hadi jumamosi ijayo.