Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo aachiwa kutoka kizuizini
16 Mei 2025Matangazo
Hayo yameelezwa na ofisi ya rais wa Angola kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Facebook ikiambatana na picha zinazomwonesha Bongo akikaribishwa kwenye uwanja wa ndege mjini Luanda.
Imesema kuachiwa kwake kunafuatia mazungumzo kati ya Rais Joao Lourenco wa Angola na kiongozi mpya wa Gabon Brice Oligui Nguema.
Bongo, ambaye familia yake iliitawala Gabon kwa miaka 55 aliondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi Agosti 2023.
Tangu wakati huo, yeye, mkewe na mtoto wao wa kiume walikuwa katika kizuizi cha nyumbani kwenye mji mkuu, Libreville kwa tuhuma za ubadharifu wa fedha za umma.