Sheria na HakiBrazil
Bolsonaro ashtakiwa kwa jaribio la mapinduzi Brazil
19 Februari 2025Matangazo
Mwendesha mashtaka wa Brazil ameenda mbali zaidi na kuthibitisha kuwa kiongozi huyo wa zamani wa Brazil pamoja na mgombea mwenza wa nafasi ya makamu wa rais Walter Braga Netto, walifahamu na kukubali mpango wa kumuua kwa kutumia sumu Rais Lula Da Silva baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa mwaka 2022.