SiasaArgentina
Rais wa zamani wa Argentina aamriwa kulipa mamilioni
16 Julai 2025Matangazo
Kirchner, mwanasiasa wa mrengo wa kushoto aliyeitawala nchi hiyo ya Amerika ya Kusini kuanzia mwaka 2007 hadi 2015, alishindwa mwezi uliopita katika rufaa yake aliyokata kwenye Mahakama ya Juu kupinga kutiwa hatiani kwa makosa ya rushwa.
Uamuzi wa mahakama hiyo uliunga mkono hukumu ya kifungo cha miaka 6 na zuio la maisha kwa Kirchner kushiriki siasa nchini Argentina.
Mwanasiasa huyo hivi sasa anatumikia adhabu yake katika kifungo cha nyumbani. Mahakama imeamuru iwapo Kirchner na wenzake watashindwa kulipa kiwango hicho cha fedha mali zao zitataifishwa.